MGALU AMPONGEZA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KWA MIRADI YA AFYA

 Na Shushu Joel, Kisarawe. 


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa jinsi ambavyo amekuwa mkombozi mkubwa katika kutatua changamoto za miradi ya Afya Nchini. 

Mbunge wa Mkoa wa Pwani Subira Mgalu akitabasamu na mtoto mchanga mara baada ya kutembelea hodi ya wazazi katika hospital ya kisarawe( NA SHUSHU JOEL)

Pongezi hizo zimetolewa na Mbunge wa viti maalumu kutokea Mkoani Pwani Bi Subira Mgalu alipotembelea katika hospital ya wilaya ya Kisarawe. 


Akizungumza mara baada ya kufika hospital hapa Mgalu alisema kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amejithatiti katika kuhakikishi wananchi wanapata kheri katika kuhakikisha Afya zao zinakuwa bora kwa upatikanaji wa huduma za kutosha kwa jamii.


"Nimetembelea hospitali ya Kisarawe kwa kweli Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa sana za maendeleo nadhani  kila mmoja analiona hili" Alisema Mbunge wa Mkoa Bi, Subira Mgalu.


Aidha Mgalu  aliongeza kuwa kwa kilichofanyika wilaya ya Kisarawe ni nchini nzima maendeleo hayo yamefanyika huku lengo likiwa ni kumaliza kabisa changamoto zinazowakabili watanzania katika sekta ya Afya. 


Pia Mbunge huyo wa Mkoa amewataka watumishi na Wananchi kuwa waangalizi wa miradi hiyo mikubwa ambayo Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

 kuweza kuilinda ili kizazi kijacho kiweze kunufaika nayo kwani hii ni historia kubwa ambayo Rais wetu ameiweka.


Naye Asia Madima ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania ( UWT) wilaya ya Kisarawe Mkoani wa Pwani amempongeza Mbunge wa Mkoa Bi Subira Mgalu kwa jinsi ambavyo amekuwa akimsemea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa yale mazuri ambayo amekuwa akitafanya nchini.


Aidha amemuomba kuwasilisha salamu za Wanawake wa wilaya ya Kisarawe huku akisema kuwa muda utaongea.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments