“UMOJA NA MSHIKAMANO NI NGUNZO YA USHINDI” MWENYEKITI WA UWT PWANI

Na Shushu Joel,Kibaha

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania ( UWT) Mkoa wa Pwani Bi, Zaynab Matitu Vulu amewataka wana chama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuendeleza umoja na Mshikamano ili kuweza kuwa wamoja kama ilivyokuwa kwa waasisi wa chama  hicho ili kuhakikisha wanashinda  kwa kishindo uchaguzi  wa serikali za mitaa2024.

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Kibaha Mjini ambapo amesema kuwa panapokuwepo na umoja na mshikamano ushindi ni lazima.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Bi, Zaynab Matitu Vulu akisisitiza jambo mbele ya wajumbe katika moja ya vikao vyake( NA SHUSHU JOEL)

“ Ni muhimu kuwa wamoja ndipo tutaweza kufanikiwa kwa mahitaji yetu hivyo niwaombe kila mmoja kwa nafasi yake kuweza kumpenda mwenzake ili kujenga mshikamano” Alisema Vulu.

Aidha alisema kuwa kama hakuna umoja na mshikamano changamoto zitakuwa nyingi hivyo waendelee kushikamana lengo likiwa ni kushinda uchaguzi huo na kwamba pasipo kuwa na nyenzo hizo ushindi hautopatikana.

Alisema kuwa kulingana na ratiba ya Taifa kuna uchaguzi mkuu katika ngazi za serikali za mitaa hivyo ni muhimu kuweza kuwa na Umoja, mshikamano na upendo kitu ambacho kitatusaidia kushinda kwa kiwango cha hali ya juu.

Akisoma taarifa fupi kwa Mwenyekiti huyo wa Mkoa Katibu UWT wa wilaya hiyo Bi, Mariam Mugasha amemsifu mwenyekiti huyo kwa jinsi ambavyo amekuwa akisisitiza uwepo wa umoja, Upendo na mshikamano kwa wana CCM.

Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wao 

Aidha aliongeza Katibu alisema kuwa atahakikisha maelekezo ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa yanafuata na kufanyiwa kazi ili kuweza kuongeza asilimia ya ushindi kwa chama chetu.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments