CCM WAMPA TANO ULEGA.

 Na Shushu Joel, Mkuranaga 

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mkamba wilayani ya Mkuranaga Mkoani Pwani wamempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega kwa jinsi ambavyo amekuwa kiongozi muongoza njia ya maendeleo. 

Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdalla Ulega akisalimia na baadhi ya viongozi wa CCM kata ya Mkamba( NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza kwenye kikao cha kamati kuu ya kata ya Mkamba katibu wa ccm kata hiyo Said Rashid  alisema kuwa kata ya Mkamba ilikuwa na changamoto nyingi ambazo zote sasa zimebaki kuwa ni historia .


Alisema kuwa Mbunge Ulega amekuwa ni nguzo kubwa katika chachu ya ukuaji wa haraka kwa maendeleo ya kata yetu ya Mkamba. 


Aidha amemuomba Mbunge huyo kuendelea kuwa na moyo huo wa usukumaji wa maendeleo katika Jimbo la Mkuranga ambalo linazidi kufunguka siku hadi siku.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewapongeza wanachama hao kwa jinsi ambavyo wamekuwa wasimqmizi wazuri wa miradi yote ambayo tumekuwa tukiifanya.


Aidha Ulega alisema ataendelea kufanikisha miradi ya maendeleo katika Jimbo la Mkuranga ili kuondoa changamoto mbalimbali. 


" Tuendelee kumuombea Dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ili azidi kutuletea maendeleo kama ilivyo dhamira yake katika Taifa hili" Alisema Ulega. 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments