UWT PWANI WAZIDI KULAANI UKATILI.

 Na Shushu Joel, Bagamoyo.

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani Bi Zaynab Matitu Vulu sambamba na  kamati ya utekelezaji ya Mkoa huo wamezidi kupinga vitendo vya ukatili kwa vitendo katika Mkoa huo.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Msata juu ya ukatili ( NA SHUSHU JOEL)

Hayo wameyasema walipokuwa Wakizungumza na Wanafunzi wa kidato cha pili na cha Nne katika shule ya Sekondari ya Msata.


  Akizungumza na Wanafunzi hao Bi, Vulu alisema kuwa kutokana na kukithiri kwa ukatili nchini jeshi la UWT  Mkoa wa Pwani limeamua kupita baadhi ya shule na kuzungumza na baadhi ya wanafunzi ili kusambaza elimu hiyo kwa wepesi.


Naye Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa UWT Mkoa Fatma Mkoga alisema kuwa  ni vyema sasa Wazazi na walezi tukaacha tabia ambazo si rafiki kwa watoto wetu.


Aidha ametumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi hao kusambaza ujumbe huo kwa wenzao walioko nyumbani  ili nao wawaambie rafiki zao kwa lengo la kusambaza elimu zaidi.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments