“JUMUIYA YA WAZAZI CHACHU YA MAENDELEO CCM” MWENYEKITI WAZAZI MKURANGA

Na Shushu Joel,Mkuranga

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Juma Mahege amesema kuwa Jumuiya hiyo ni chachu ya maendeleo na malezi bora kwa watoto hapa Nchini.

Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Mkuranga Juma Mahege akisisitiza jambo kwa viongozi wa ccm.( NA SHUSHU JOEL)

 Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo alipokuwa akizungumza na wana Chama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mgawa .

Alisema kuwa Jumuiya hii ni  nguzo kubwa katika mambo mengi hivyo kila kiongozi aliye ndani ya jumuiya yetu ni muhimu kuweza kujitafakali kwa kina juu ya uwezo wake wa kuongoza na kusaidia jamii yetu katika Nyanja mbalimbali.

Aidha amewataka viongozi wa jumuiya hiyo kuendelea kuyasema yale mazuri yanayofanywa na Rais wetu wa jamhuri ya Muungno wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwani maendeleo anayoyafanya yamezidi kuwa msaada mkubwa kwa wananchi waTanzania.

 

“ Sasa hivi kuna mashule, zahanati, vituo vya Afya , miundombinu bora ,umeme, maji na mengine mengi ambayo Rais wetu amekuwa akiyafanya” Alisema Mahege’

Naye katibu wa ccm wa kata hiyo Miraji Msumi alisema Mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Mkuranga ametuachia deni kubwa wana ccm hivyo tuna mwakikishia tutafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha ccm inazidi kuwa juu kama ilivyo sasa.


Aidha amewataka viongozi kuyafanyia kazi maneno yaliyosemwa na mwenyekiti wa Wazazi ili kuweza kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Pia katibu huyo amempongeza mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Abdallah Ulega kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa katika ufanisi wa ufanikishaji wa maendeleo katika kata hiyo kwani awali kata hiyo ilikuwa nyuma sana lakini sasa hivi tunaweza kusema kuwa Ulega ni mfano wa kuigwa.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments