Na Shushu Joel, Kibaha Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Pwani Alhaji Mussa Mansour akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi madawati 100 katika wilaya ya Kibaha( NA SHUSHU JOEL)
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Pwani Ndugu Shabani Mlawa amempongeza Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa huo Alhaji Mussa Mansour kwa jinsi ambavyo amekuwa akijitolea kukisaidia Chama na Serikali ya Mkoa huo.
Hayo ameyasema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbalimbali katika mahojiano mara baada ya zoezi ya kukabidhiwa kwa madawati 100 kwa wilaya ya Kibaha na Mjumbe huyo.
Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa alisema kuwa Alhaji Mansour amekuwa tunu kwa Mkoa wetu kutokana na matendo yake ya kuwa kinara namba moja katika uchangiaji wa miradi ya Chama na ile ya Serikali.
" Halmashauri ya Kibaha mji imepokea madawati 100 kwa ajili ya wanafunzi wetu kitu ambacho kinakwenda kuwasaidia watoto wetu kuondokana na changamoto ya kukaa chini iliyokuwa ikiwakabili" Alisema Mwenyekiti wa CCM Mkoa
Aidha Mwenyekiti huyo wa CCM amewataka watu kuiga mfano wa Alhaji Mansour kwa jinsi anavyojitoa kusaidia matatizo mbalimbali ya jamii.
" watu wenye Roho kama za Alhaji Mansour Mungu anawaongezea na kuwanyanyua kuwa juu hivyo kutokana na jinsi Alhaji Mansour anavyojitoa sie tunamuombea aweze kukua zaidi ya hapo alipo sasa " alisema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Shabani Mlawa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kibaha Nicki amemsifu Alhaji Mansour kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuchangia maendeleo
Hivyo mambo ya maendeleo sio ya kisiasa hivyo kila mwenye nafasi anakaribishwa kuleta miradi hiyo.
MWISHO
0 Comments