NA MWANDISHI WETU
Maneno hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Mh. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Bwilingu katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Bwilingu.
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete katikati akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Ramadhani Poss |
Mbunge aliyasema hayo akiwahamasisha wananchi kuendelea kushiriki maendeleo na kuwa ukombozi wa maendeleo ni msingi unaotakiwa kusimamiwa na wananchi wenyewe wa Halmashauri ya Chalinze.
Akimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo , ndugu Kikwete alimshukuru yeye na watumishi wa halmashauri katika kutekeleza maelekezo yanayotolewa kwenye vikao ususani ni ujenzi wa mji wa Chalinze na maeneo ya huduma muhimu za wananchi haswa katina sekta ya maendeleo ya jamii ususani ni Soko, Kituo Cha Afya, Mashule, miundombinu ya barabara , n.k
0 Comments