ALHAJI MANSOUR ATOA MILIONI 2 KWA AJILI YA UMALIZIAJI WA MSIKITI

 Na Shushu Joel, kibaha.

MJUMBE wa kamati ya siasa Mkoa wa Pwani Alhaji Mussa Mansour ametoa kiasi cha Shilingi Milioni mbili katika msikiti wa Masjid.muhajirina uliopo Kongowe wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani ili zisaidie katika umaliziaji wa msikiti huo.

Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Pwani Alhaji Mussa Mansour akikabidhi fedha tasilimu milion 2 kwa imamu wamsikiti kwa ajili ya umaliziaji wa msikiti huo( NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Alhaji Mansour alisema kuwa ni vyema tukajijengea tabia ya utoaji kwa jamii ili tuweze kuongezewa na Mwenye Mungu.

Alisema kuwa Waislam tumekuwa nyuma sana katika utoaji wa sadaka hivyo sasa tunapaswa kubadilika ili tuweze kusaidia misikiti na kusaidia jamii kwa ujumla kama wanavyofanya wenzetu.

Aidha amewakumbusha waumini  wa dini zote nchini kuendelea kumuombea Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwani ndiye Rais wa kwanza Mwanamke lakini anafanya mambo makubwa mpaka dunia inamshangaa


Aidha Mjumbe huyo wa kamati ya siasa amewakumbusha wazazi na Walezi kuendeleza maadili mema kwa vijana wetu ili hapo baadae waje kuwa msaada mkubwa kwa Taifa  letu.

Naye Kiongozi wa msikiti huo Juma Ally amempongeza Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Pwani Alhaji Mussa Mansour kwa matoleo yake katika msikiti huo wa Masjid.muhajirina kwani pesa hizo zinakwenda kubadili muonekano uliopo na kuleta muonekana mpya na wa kipekee katika msikiti huo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments