Na Shushu Joel, Bukombe.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndugu Nelvin Salabaga amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa wananchi.
![]() |
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Bukombe akiwaaga wajumbe mara baada ya mkutano( NA SHUSHU JOEL) |
Haya ameyasema alipokuwa akizungumza na viongozi na wana Chama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Bulangwa kwenye mwendelezo wa ziara kwa viongozi hao wa Jumuiya zote ikiwemo Wazazi ,Uwt na Uvccm.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa Mbunge wetu amefanikiwa kuwakosha Wananchi wote wa Jimbo kwa kupeleka Maendeleo katika kila kata kwa lengo la kurahisisha mahitaji ya muhimu ya Wananchi wa Jimbo la Bukombe.
![]() |
Wajumbe wakisikiliza maneno ya hekima kutoka kwa mwenyekiti wa vijana |
Mbali na hilo Mwenyekiti huyo wa Vijana amewataka Wananchi kuendelea kumuunga Mkono Dkt Biteko kwani amekuwa ni kiongozi wa pekee katika jimbo hilo kwa kiongozi ambaye amekuwa akifanya kazi za kuwapa Maendeleo wananchi na si maneno maneno .
Naye Peter Masunga amempongeza Mbunge kwa kusema na kutenda kwa vitendo kwani hii ilikuwa kiu ya wananchi wa Bukombe ambao muda mrefu walikuwa wakihitaji Maji,Umeme,Afya na miundombinu iliyokuwa ni changamoto kubwa kubwa kipindi cha nyuma.
0 Comments