Na Shushu Joel, Bukombe.
WANAWAKE wa kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamempongeza Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Dotto Biteko kwa kufanikisha kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma muhimu ya maji.
![]() |
Mbunge wa jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu waziri Mkuu akifafanua jambo mbele ya Bunge la Tanzania |
Akizungumza na HABARI MPYA MEDIA Bi, Ester Charles alisema kuwa kipindi cha nyuma hupatikanaji wa maji ilikuwa ni janga sana katika kata yetu kwani tulikuwa tukitumia muda mwingi kwenda kutafuta maji ya kutumia.
¹ Ndoa zetu zilikuwa na changamoto sana kutokana na Wanawake wengi kuwa tunaamoa alfajiri sana na kuwaacha wanaume zetu kitandani peke yao ila sasa hivi tunalala nao mpaka saa moja " Alisema Bi, Ester .
Moja ya matank ya maji yaliyopo katika kata za ndani ya wilaya ya Bukombe ( NA SHUSHU JOEL) |
Aidha amewaomba wananchi wote wanaotumia maji hayo kuendelea kutunza miradi tunayoletewa na serikali ili kizazi chetu kiendelee kunufaika na maji hayo kwani tulikuwa na changamoto kubwa lakini sasa tunayo hivyo ni lazima tuyatunze yatutunze.
Kwa upande wake Meneja wa Maji kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndg Shija Joshua amempongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kushusha fedha kwa ajili ya miradi mingi ya maji na inayozidi kutekelezeka kwa kasi.
Aidha amewataka wananchi kuendelea kuunganishwa na miradi ya maji majumbani ili iwe vyepesi kupata huduma hiyo wakiwa majumbani .
MWISHO
0 Comments