CCM BUKOMBE YAVUNJA NGOME YA CHADEMA.

 Na Shushu Joel, Bukombe 

CHAMA Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kimeibomoa ngome ya CHADEMA kwa kuvuna wanachama wa Chama hicho zaidi ya 20 ambao wamerudisha kadi na kujiunga na CCM. 

Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Bukombe Hassan Abdalah akipokea kadi


Akizungumza wakati wa kukabidhiwa kadi hizo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndugu Hassan  Abdalah alisema kuwa ni jambo jema watanzania kutambua kipi ni chama sahihi na Chenye kutoa  huduma bora kwa jamii.


" Kwa utendaji huu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan wengi sana watarudisha kadi na watajiunga na CCM " Alisema Mwenyekiti huyo wa Wazazi Wilaya hiyo Ndugu Hassan 


Aidha amewapongeza wale wote walioamua kufanya maamuzi sahihi ya kurudi Chama dume, Chama chenye uchu na maendeleo ya wananchi wake.


Kwa upande wake Mmoja wa waliorudisha kadi za CHADEMA  na kujiunga na CCM  Ndugu Matoja Juma alisema kuwa walichelewa sana kuwe kwenye Chama chenye busara na hekima na chenye kusikilizana.


Aidha amewataka Watanzania kujiunga na CCM kwani ni chama chenye kuleta maendeleo kwa watanzania na wala sio maneno maneno.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments