Na Shushu Joel,Bukombe
MBUNGE wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko amezidi kuwana kinara wa kutafasiri kauli mbiu ya wananchi wa jimbo hilo ya kusema na kutenda (KNK) kwa vitendo Zaidi
Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko akifafanua jambo
Wakizungumza
kwa wakati tofauti tofauti wananchi wa jimbo hilo wamempongeza Dkt Biteko kwa
kufanikiwa kwa asilimia kubwa kwa uwakilishi wake wa wananchi katika Bunge la
Jmahuri la Muungano wa Tanzania.
Amina Hamis(46)
ni mkazi wa kata ya Uyovu mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari
alisema kuwa Jimbo la Bukombe limepiga hatua kubwa katika maendeleo hii ni
kutokana na uongozi bora unaoonyeshwa na Mwakilishi *Mbunge Dkt Biteko) kwani
amefanikiwa kutuvusha wananchi wake.
Aidha
alisema kuwa hata uchumi wa wakazi wa Bukombe umekuwa sana na hii ni kutokana
na uwepo wa miundombinu ya barabara ya uhakika na yenye kupitikana wakati wote
hivyo usafirishaji wa mazao umekuwepo kwa wakati na kupelekea wananchi kupata
fedha.
Naye Juma
Manamba(67) amesema kuwa Dkt Biteko amefanikiwa kututimizia mahitaji yetu
wananchi wa Bukombe kwani kile ambacho tulikuwa tukikihitaji kimefanyika kwa
vitendo.
Aliongeza
kuwa mengi yametendeka katika jimbo la Bukombe chini ya Dkt Biteko yote haya
yanatokana na upendo wake mkubwa kwa jamii ndio maana maendeleo yanazidi
kufanyika kwa haraka sana’
MWISHO
0 Comments