“TUTAMLINDA DKT BITEKO KAMA MBONI” UVCCM GEITA

Na Shushu Joel,Bukombe

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita (     UVCCM) umeapa kumlinda kwa hali na mali Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Nishati ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa utaendelea kumlinda kutokana na kuwa Dkt Biteko ni Mboni ya jicho katika Mkoa wa Geita.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa baraza la umoja huo(NA SHUSHU JOEL)


Akizungumza mara baada ya kikao cha Baraza la jumuiya hiyo Mwenyekiti wa  UVCCM Mkoa wa Geita Manjale Magambo alisema kuwa  Rais wa Jamhuri wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametuheshimisha sana wananchi wa Mkoa wa Geita kwa kumteua Mhe. Dkt Dotto Mashaka Bitekonkuwa Naibu Waziri Mkuu hivyo ni zamu yetu kuhakikisha Dkt Biteko analindwa kama mboni ya macho zetu.


Aidha aliongeza kuwa Biteko amekuwa ni kiongozi wa pekee na wa kuigwa katika Taifa letu kwani amekuwa msimamizi na mtendaji mzuri katika kuhakikisha maendeleo ya wananchi yanapatikana kwa haraka ili kuondoa changamoto zinazowakabili.


Hivyo amemtaka Dkt Biteko kupiga kazi bila wasiwasi ya aina yeyote ile kwani Umoja wa Vijana tumeamua kumlinda ili atuletee maendeleo sisi wananchi wa Bukombe na Geita kwa ujumla.



Naye Mjumbe wa baraza hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Bukombe Nelvin Salabaga alisema kuwa Dkt Biteko amekuwa ni kiongozi wa maendeleo na sio kiongozi wa maneno maneno hivyo Vijana wa Bukombe tunamatumaini m,akubwa ya kuendelea kupata maendeleo kutoka kwa Mbunge wetu Biteko.


Aidha amempongeza Dkt Biteko kwa ufanisi wa ujenzi wa ofisi ya CCM ya Wilaya ambayo sasa inazidi kuipa heshima Bukombe

MWISHO

Post a Comment

0 Comments