Na Shushu Joel, Bukombe
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Bi' Julieth Simon amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko kwa kuzidi kuipambania elimu ili iweze kukua jimbo humo.
![]() |
Dkt Biteko akifafanua jambo katika moja ya mikutano yake |
Akizungumza mara baada ya kikao kazi Mwenyekiti huyo alisema kuwa Jimbo la Bukombe limefanikiwa kuwa na wabunge wengi lakini Dkt Biteko amezidi kuwa kiongozi wa pekee kwa ufanisi wa hali ya juu kwa maendeleo ya wananchi.
Aliongeza kuwa shule za msingi na sekondari zimezidi kuongezeka zaidi kwa kusudi la kukuza elimu kwa watoto wetu jambo ambalo Mbunge Dkt Biteko analifanya kwa vitendo.
" Nchi inapoongeza maarifa kwa watu wake basi ujue uchumi wa Taifa hilo unakwenda kuongezeka mara dufu na pia kufungua fursa mbalimbali" Alisema Mwenyekiti wa UWT Bi, Julieth.
Naye Monika Juma amempongeza Mwenyekiti huyo kwa kuonyesha wananchi kile ambacho kinafanywa na mbunge wetu ambaye amekuwa akijitolea kwa asilimia kubwa ili kuhakikisha wananchi wa Bukombe wanapata kile kinachostahili kupata katika nyanja ya maendeleo.
MWISHO
0 Comments