KATIBU WA CCM BUKOMBE ASHUSHA NONDO KWA MAKATIBU.

 Na Shushu Joel, Bukombe.


KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndugu Leonard Mwakalukwa amewapa somo makatibu kata wa Chama hicho juu ya umuhimu wa wanachama kuwa na kadi za electronik..

Katibu wa CCM akitoa maelezo kwa moja wa makatibu kata( NA SHUSHU JOEL)


Akizungumza katika kikao kazi hicho Katibu huyo alisema kuwa ni jambo la muhimu sana kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuweza kutambua kuwa Chama Chao kinawadhamini sana na ndio maana kimewaletra kadi hizo ambazo zinafaidi lukuki kwao.


Aidha alisema kuwa moja ya kuwa na kadi hizo ni kuingia katika mfumo wa Chama jambo ambalo linaondoa mkanganyiko mkubwa wa mwingiliano wa namba za kadi pia urahisi wa mfumo wa malipo kwa kadi yako.


Pia amewakumbusha maafisa Tehema wa wilaya na wale wa kata kuhakikisha wanakwenda majumbani na kwenye vikao kuwasajili wana CCM ambao wana kiu ya kuwa na kadi za kielectronik .


Naye Katibu kata wa kata ya Runzewe Mashariki Anold Mhozwa amempongeza katibu wa CCM wilaya kwa jinsi ambavyo amezidi kuwa chachu kwa viongozi na hasa katika juwakumbusha wajibu wao wa kila siku kitu ambacho kimezidi kuchangia ukuaji wa Chama kila kukicha.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments