"DKT BITEKO CHANZO CHA KUIMALIKA HUDUMA ZA AFYA BUKOMBE " Dr. MKAPA

 Na Shushu Joel, Bukombe 

MGANGA Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Dr. Deograsia Mkapa amesema kuwa tangu Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu achukue nafasi hiyo ya kuwa mwakilishi wa wananchi kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta ya Afya.


Hayo amesema alipokuwa katika zoezi la upimaji wa magonjwa ambayo sio ambukizi kama vile kisukali,tezi dume,na pressure kwa wakazi wa kata ya Bulangwa ambapo zoezi hilo lillikuwa likifanywa bure.


Aliongeza kuwa watu wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kupima magonjwa hayo na kuchangia damu kitu ambacho kimekuwa kikitupatia faraja kubwa watoa huduma za Afya .


Aidha alisema kuwa kumekuwa na msaada mkubwa sana wanaoupata kutoka kwa mbunge Dkt Biteko na hii ndio maana tumekuwa tukifanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu.


"Bukombe kwa sasa kuna vituo vya afya 7, Hospital 1 na zahanati 17 hiyo ni hatua kubwa sana katika idara yetu ya Afya hivyo pongezi zimfikie Mbunge Dkt Biteko " Alisema Mganga Mkuu Dr. Mkapa.


Pia zoezi hilo la upimaji wa magonjwa hayo limefanikisha upatikanaji wa damu chupa zaidi 70 na kupima watu 478.


Naye Nyanzara Masalu  (57) amewashukuru jopo la watu wa Afya kwa kufanya zoezi la upimaji wa magonjwa mbalimbali.


Aidha amewaomba wananchi wenzake kuchangamkia fursa kama hizi pindi zinapotangazwa kwani kutambua Afya yako ni kitu cha muhimu sana kwa binadamu.


MWISHO


Post a Comment

0 Comments