UWT WAAHIDI MAKUBWA KWA DKT BITEKO.

 Na Shushu Joel, Bukombe 

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)  Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita umeahidi kumpigia kura za kishindo Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko ili azidi kuendelea kuwa kiongozi wa jimbo hilo.

Baadhi ya wanawake wilaya ya Bukombe wakifurahia jambo katika sherehe za kuzaliwa kwa CCM( NA SHUSHU JOEL)

Maneno hayo yamesemwa  na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Geita Bi' Lorensia Bukwimba alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya kutimiza miaka 47 kwa kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) ambapo kimkoa jumuiya hiyo iliyafanya katika ukumbi wa CCM wilayani Bukombe.


Aliongeza kuwa ni vyema wanawake kutambua thamani kubwa ya maendeleo inayofanywa na mbunge wa jimbo la Bukombe Dkt Biteko kwani ni muda mchache lakini maendeleo yaliyopigwa ni makubwa.


" Wanawake wenzangu niwakumbushe kuendelea kuwaombea viongozi wetu ambao wanalifanyia maendeleo makubwa Taifa hili" Alisema Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Geita Bi Lorensia 


Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwafanikishia watanzania maendeleo yale ambayo walikuwa na kiu nayo kwa muda mrefu.


Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Bukombe Teddy Mageni amemwakikishia Mwenyekiti huyo kuwa jumuiya hiyo imejipanga kisawasawa kuhakikisha Dkt   Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wetu Dkt Biteko wanapata heshima kubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa CCM kushinda kwa kishindo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments