Na Shushu Joel, Bukombe
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM) Ndugu Fakii Lulandala ametoboa siri kubwa waliyokuwa wameipanga ya kutaka kumpa Urais wa Chama Cha Walimu Dkt Dotto Biteko kipindi hicho.
![]() |
Katibu Mkuu wa Uvccm Lulandala akisisitiza jambo (NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza na baadhi ya viongozi mbalimbali wa Chama na Jumuiya zake wa wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Katika huyo wa umoja wa Vijana Ndugu Lulandala alisema kuwa Wananchi wa Bukombe mnabahati kubwa sana ya kuwa na kiongozi mwenye maona ya mbali na mwenye hofu ya Mungu hivyo endeleeni kumpa ushirikiano mkubwa ambao matunda yake mtazidi kuyaona .
" Wakati nikiwa Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Mbeya tulikubaliana kumpa Dkt Biteko Urais wa chama chetu kutokana na uwezo wake mkubwa alionao lakini kumbe na wananchi wa Bukombe wanampango wa kumpa ubunge na wakafanikiwa" Alisema Katibu Mkuu Uvccm Taifa Lulandala
Aidha aliongeza kuwa Dkt Biteko ni kiongozi msikivu sana na ndio maana hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amemuongeza nafasi ya kuwa Naibu Waziri Mkuu.
Pia Lulandala amemsifu kwa ushawishi na mchango alioutoa kwenye ujenzi wa ofisi ya CCM Wilaya ambayo kwa nchi nzima hakuna ofisi kama hii .
Naye Katibu wa CCM wilaya ya Bukombe Leonard Mwakalukwa amempongeza katibu wa Uvccm Taifa kwa utendaji wa kazi mkubwa na uliotukuka anaoufanya katika jumuiya hiyo.
Aidha alisema kuwa uvccm imepata mtendaji mwenye uchu wa maendeleo hivyo jumuiya hiyo inakwenda kubadilika sana.
MWISHO
0 Comments