"DKT BITEKO KATUFAGILIA NJIA YA USHINDI WA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA" SALABAGA

 Na Shushu Joel, Bukombe

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM)  Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndugu Nelvin Salabaga amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi wa Bukombe kutembea kifua mbele kwa utekelezaji mkubwa wa maendeleo unaofanywa na Mbunge wa Jimbo hilo.

Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Bukombe Nelvin Salabaga akizungumza na waandishi wa habari( NA SHUSHU JOEL)

Hayo amesema alipokuwa akizungumza na na Wanachama wa Chama hicho kuanzia na wananchi wa kata ya Busonzo Wilaya Bukombe katika moja ya mikutano ndani ya kata hiyo ambayo yeye ni mlezi.

Aliongeza kuwa katika Jimbo la Bukombe hatuna uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na kile kilichokuwa kikihitaji kifanyika kwa wananchi wa Bukombe kimefanikiwa kufanyika kwa asilimia kubwa.

Aidha Mwenyekiti Salabaga alisema kuwa wao kama umoja wa vijana wanampongeza sana Mbunge ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko kwa kuwaondolea uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na utendaji wake wa ufanisi wa hali ya juu katika uletaji wa miradi ya maendeleo. 

" kwa kweli Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bukombe tunamsifu sana Dkt Biteko kwa kutusafishia njia ya kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa " Alisema  Salabaga 

Naye Diwani wa kata hiyo  Safari Mayala amempongeza Mwenyekiti wa Uvccm wilaya kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele kwa kuelezea yale yanayofanywa na viongozi wetu.

Aidha Diwani huyo alisema kuwa wananchi wa Jimbo la Bukombe ni waelewa na wanaona kile wanachotendewa na viongozi waliowachagua kwa ajili ya kuwawakilishi Bungeni ,kwani Dkt Biteko amekuwa ni nguzo kubwa ya maendeleo katika Jimbo letu.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments