Na Shushu Joel, Geita.
MBARAZA wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Geita Ndugu Reuben Sagayika amewang'ata vijana wa Mkoa huo kuendelea kuwa wabunifu wa miradi yao ambayo itawaongezea kipato cha kuendesha maisha yao.
![]() |
Mbaraza kushoto akiteta jambo na Mwenyekiti Uvccm wilaya ya Bukombe(NA SHUSHU JOEL) |
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na vijana wa wilaya ya Bukombe katika Baraza lililofanyika katika ukumbi wa CCM.
Aliongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amezidi kuwa chachu ya maendeleo ya vijana nchini hivyo ni zamu yetu vijana wa Mkoa wa Geita kuhakikisha tunachangamkia fursa hizo.
" Kwa hapa Wilaya ya Bukombe mnaweza kuanzisha hata ufugaji wa nyuki kitu ambacho kinawezekana kutokana na mazingira ya Bukombe kuwa na misitu na mito ya kutosha na mimi kama mbaraza wenu nitawasaidia kwa hali na mali kuhakikisha mnafanikisha" Alisema Mbaraza Sagayika
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Bukombe Ndugu Nelvin Salabaga amempongeza Mbaraza huyo kwa upendo wake wa dhati kwa Jumuiya hiyo na hasa katika kuwainua Vijana kiuchumi.
Aidha Mwenyekiti huyo amemwakikishia Mbaraza huyo kuwa muda si mrefu atapata maombi yao ili waweze kuanzisha mradi ambao utakuwa chachu ya maendeleo kwa Jumuiya hiyo.
MWISHO
0 Comments