Na Shushu Joel, Bukombe
JUMUIYA ya Umoja wa Wazazi wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamepania kutembea kaya hadi kaya kuwahamasisha wananchi kuweza kushiriki kikamilifu katika zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa.
![]() |
| Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Bukombe Hassan Mohamed akisisitiza jamo kwa viongozi wa jumuiya hiyo(NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza na viongozi wa jumuiya hiyo wa ngazi za kata Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wilaya ya Bukombe Ndugu Hassan Mohamed alisema kuwa ushiriki wetu wa dhati katika uchaguzi huo kwa lengo la kukipatia ushindi wa kishindo Chama Cha Mapinduzi (CCM) .
Aidha Mwenyekiti huyo amewakumbusha viongozi wa kata kuendelea kumsemea Mbunge wetu Dkt Dotto Biteko kwa jinsi ambavyo amekuwa kinara katika maendeleo na utatuzi wa changamoto za wananchi.
" Kama Jumuia ya wazazi tumekubaliana kumheshimisha Mbunge wetu Dkt Biteko na Rais wetu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan SSH) kwa kuwapatia viongozi wanaotokana na CCM katika uchaguzi huo" Alisema Hassan
![]() |
| Wajumbe wakifuatilia ajenda za mkutano wa wazazi wilayani Bukombe |
Naye mjumbe wa Baraza la wazazi wilaya hiyo Bi, Mariana Genya amemwakikishia Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kuwa wao kama wazazi watahakikisha hakuna mtaa, kijiji na kitongoji kitakachopotea katika wilaya ya Bukombe.
Aliongeza kuwa wananchi wa wilaya ya Bukombe ni waelewa na wanatambua jinsi gani CCM inavyowafanyia mambo makubwa ya maendeleo.
Hivyo kutokana na jinsi Mbunge wetu ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa Jimbo la Bukombe hakuna kilichosimama" Alisema Bi, Marianas
MWISHO


0 Comments