NA SHUSHU JOEL, SINGIDA
Afisa Vijana Mkoa wa Singida Ndugu Frederick Ndahani amewataka Vijana wa Chama cha Skauti Wilaya na Mkoa kwa ujumla kuimarisha utunzaji wa Mazingira ili kukabiliana na mabadiriko ya Tabia ya Nchi.
Ndahani ambaye pia ni Kamishina wa Skauti Wilaya ya Singida amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mwanzilishi wa Skauti Duniani Sir Robert Steven simith Baden Powell yaliyofanyika Kiwilaya katika Viwanja vya Bombadia Manispaa ya Singida.
Ndahani amesema Chama cha Skauti kitaendelea kuwajenga Vijana katika maadili mema,uwajibikaji na uzalendo kwa Taifa na kuwaomba Wazazi na Walezi kuwaruhusu Wanafunzi kujiunga na Chama cha Skauti.
Katika kuunga mkono Serikali Ndahani amewagiza Vijana kupanda na kutunza Miti ili kuendelea kuboresha Mazingira katika Mkoa na Taifa letu.
Aidha Ndahani ameelekeza kila kundi la Skauti kwa Shule za Msingi na Sekondari kuhakikisha wanakuwa na Miradi ya Bustani za mboga mboga na vitaru vya Miti ili kuimarisha Elimu ya kujitegemea Shuleni itakayo saidia uendeshaji wa Makundi badala ya Kuomba uwezeshwaji kutoka kwa Wazazi na Walezi.
Ismail Ayoub Saganka Kiongozi wa Makundi Chama cha Skauti Manispaa watasimamia upandaji na kuitunza wa Miti hiyo ili iweze kukua,Ipo desturi kupanda miti mingi na kuiacha ambapo hufa au kuliwa na Mifugo hivyo Malengo ya uboreshaji wa Mazingira kutokufikiwa.
Kwa upande wake Sabrina Mohamed Rashidi Kiongozi Msaidizi wa Makundi amemushukuru Afisa Vijana ambaye pia ni Kamishina wa Wilaya kwa kuungana na Vijana katika Maadhimisho ya Mwanzilishi wa Skauti Duniani na kuahidi kuyafanyia kazi Maelekezo yaliyotolewa.


0 Comments