Na Shushu Joel, Bukombe
MWENYEKITI wa Chma Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndugu Matondo Lutonja amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia nia Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika mafanikio ya chama katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo ambazo awali ilikuwa ni ndoto lakini kipindi chake mambo yamezidi kuwa mbele.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko akifafanua jambo mbele ya wajumbe ambao hawapo pichani.( NA SHUSHU JOEL)
Hayo amesema
alipokuwa akizungumza na mabalozi wa wilaya hiyo katika ukumbi wa ccm wa
wilaya.
Aliongeza
kuwa Dkt Biteko amekuwa msaada mkubwa katika maendeleo ya chama na mpaka hapo
tulipo sasa zimetrumika nguvu nyingi kutoka kwake .
Aidha
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ni vyema kila kiongozi aliyepewa dhamani na
chama cha mapinduzi kuhakikisha anawajibika kwa bidii na kuwa msaada mkubwa kwa
kuwatumikia wananchi vile wanavyohitaji .
“Dkt Biteko
amekuwa kiongozi wa pekee katika kukisaidia chama na hiki ndio chnazo cha
kuzidi kuvuna wapinzani katika sehemu mbalimbali”Alisema Mwenyekiti Lutonja.
Kwa upande
wake mmoja wa mabalozi mzee Ally Juma
alisema kuwa hakuna asiyeona kile kinachofanywa na Mbunge wetu katika Nyanja ya
maendeleo wilayani kwetu hivyo uongozi wa Dkt Biteko mumekuwa msaada mkubwa kwa
wananchi wa Bukombe.
MWISHO
0 Comments