BUKOMBE YAIBUKA KIDEDEA UVCCM CUP

 Na Shushu Joel, Geita.

TIMU ya Umoja wa Vijana  (UVCCM FC) ya wilaya ya Bukombe imeibuka kidedea wa mashindano hayo mara baada ya kuinyuka timu ya Uvccm Geita Dc kwa jumla ya mabao 6 kwa 5.


Katika michezo huo ambao umefanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Kalangalala.


Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika Mgeni rasmi Muhsin Ussi  ambaye ni MNEC kutokea Zanzibar alisema kuwa mashindano ya Uvccm Mkoa wa Geita yamekuwa na msisimuko mkubwa kutokana na jinsi ambavyo yamekuwa yakiendeshwa na usimamizi mzuri wa  Mwenyekiti wa Vijana wa Mkoa huo Ndugu Manjale Magambo.


" Niwapongeze Bukombe Fc kwa ushindi walioupata dhidi ya Geita hivyo wanastahili kupata hiyo zawadi ya milioni 1.5 kwani wamejituma sana uwanjani" Alisema Ussi 


Aidha ameupongeza uongozi wa chama na serikali kwenye Mkoa huo kwa umoja wanaouonyesha katika usimamizi wa miradi ya maendeleo ambapo wamepokea fedha nyingi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan. 


Pia MNEC huyo amewataka wenyeviti wa Mikoa  mingine  kuiga kile kilichofanywa na Mwenyekiti Manjale wa Geita.


Naye Mwandaaji wa mashindano hayo ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita Ndg Manjale Magambo amewapongeza Bukombe kwa ushindi wa mashindano hayo na wale wote walioshiriki katika ligi hiyo.


Aliongeza kuwa michezo ni ajira hivyo ni vyema vijana kutumia vipaji walivyonavyo ili kuweza kujipatia ajira hiyo ya mpira.


Katika mchezo huo Bukombe wamepata ushindi wa jumla ya bao 6 kwa 5mara baada ya kutoka sare ya 1 kwa 1 ndani ya dakika 90 za mchezo.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments