Na Shushu Joel, Bukombe
MBUNGE wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita Mhe. Dkt Dotto Mashaka Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu ametoa motisha kwa timu ya Umoja wa Vijana (UVCCM BUKOMBE FC kwa kutinga fainali katika mashindono ya UVCCM MKOA WA GEITA
Akizungumza kwa njia ya simu Dkt Biteko alisema kuwa amefurahisha sana na kitendo cha timu hiyo kuichapa timu ya UVCCM CHATO kwa jumla ya magoli 3-2 hivyo kufanikiwa kutinga fainali.
Aidha alisema kuwa ni vyema sasa vijana kutumia michezo hiyo kujitangaza ili waweze kufika mbali zaidi kwa kutumia vipaji walivyopewa na Mungu.
" Jimbo la Bukombe lina vijana wenye vipaji sana hivyo sasa ni wakati wa makocha na wale wenye uona wa kuona vijana kuweza kukimbilia Bukomne ili kujinyakulia vijana watakao kuwa msaada katika timu zao" Alisema Dkt Biteko Naibu Waziri Mkuu.
Pia Dkt Biteko aliongeza kuwa kwa wale walioingia fainali na timu hiyo ya UVCCM BUKOMBE wajiandae kisawasawa maana vijana wangu ni shupavu na imara sana katik a kusakata mpira wa miguu.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Ndugu Nelvin Salabaga amewasifu vijana wake kwa namna walivyojitoa kuhakikisha wanapata ushindi na kutinga fainali .
Aidha amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu kwa kuwa karibu mstali wa mbele katika kuwasaidia kwenye mahitaji mbalimbali.
MWISHO

0 Comments