Na Shushu Joel, Bukombe
MKUU wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Said Nkumba amezindua zoezi la chanjo kwa watoto kuanzia umri wa miezi tisa mpaka miaka mitano katika hospital ya Wilaya hiyo.
![]() |
Mkuu wa wilaya ya Bukombe Said Nkumba akishiriki kumshika mtoto kwa ajili ya chanja( NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza katika uzinduzi huo Nkumba alisema kuwa ni vyema wananchi wa Bukombe kuhakikisha mnawapeleka watoto katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya ili waweze kupata chanjo.
" Mtoto anapopata chanjo anakingwa na magonjwa mbalimnali ikiwemo magonjwa ya milipuko ambayo ni hatari sana kwa watoto wetu hivyo ni vyema kuwapeleka watoto kupata chanjo" Alisema Mkuu wa Wilaya Nkumba.
Aidha aliongeza kuwa wilaya inatarajia kutoa chanjo kwa watoto zaidi ya elfu sitini (60,000) ili waweze kukingwa na magongwa hayo.
Mbali na zoezi hilo Mkuu huyo wa wilaya amewataka watumishi wa sekta ya Afya kuhakikisha wanatoa huduma kwa uhakika ili watoto waweze kupata chanjo pasipo buguza yeyote ile.
Kwa upande wake mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dr. Deograsia Mkapa amemwakikishia mkuu wa wilaya kuwa zoezi hilo litaenda kama lilivyopangwa.
Aidha Dr Mkapa amewataka wananchi kuwapeleka watoto kwenye vituo vyote vinavyotoa huduma za Afya wakapate chanjo zitakazowasaidia kujikinga na magonjwa ambukizi.
MWISHO
0 Comments