DMO AKOSHWA NA WINGI WA WATOTO WANAOPATA CHANJOYA MEASCLES RUBELLA

Na Shushu Joel,Bukombe

MGANGA Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Dr. Deograsia Mkapa amewapongeza wananchi wa wilaya hiyo kwa jinsi ambavyo wamekuwa mstali wa mbele katika  kuitikia wito wa kupeleka watoto kupata chanjo ya Meascles Rubella

Mganga Mkuu wa Bukombe Dr, Mkapa akimshika mtoto ili aweze kupatiwa chanjo( NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza na baadhi ya wanawake waliojitokeza kuwaleta watoto kupata chanjo hiyo Dr Mkapa alisema kuwa zoezi hilo lina siku tatu sasa tangu kuzindiliwa kwake na Mkuu wa wilaya hiyo Ndugu Said Nkumba  lakini limezidi kuwa na  mafanikio makubwa na yenye tija kwa ujumla


Aidha amewashukuru wananchi wa Bukombe kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakijitokeza kwa mazoezi ya chanjo mara tu serikali inapowatangazia uwepo wa zoezi hilo.


Pia Dr Mkapa amemsifu Rais wa Jamhuri a Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kujali wananchi wake kwa asilimia mia ndio maana chanjo hizi zinatolewa bure kwa wananchi kweli huyu ni kiongozi wa pekee.


Naye Bi, Mwanahawa Ally amempongeza Mganga Mkuu Dr, Mkapa kwa kuwa mstali wa mbele katika kutoa na kusimamia huduma bora katika wilaya ya Bukombe Hivyo Dr Mkapa amezidi kuwa mfano wa kuigwa kwa watoa huduma jambo ambalo limekuwa likipelekea huduma kuzidi kuwa bora kila kunapokucha katika wilaya ya Bukombe.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments