“UWEKEZAJI UKO WAZI BUKOMBE” LUTENGANO

Na Shushu Joel,Bukombe

MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndugu George Lutendano amefungua milango ya uwekezaji kwa makampuni,Taasisi na watu binafsi kuweza kujitokeza kuwekeza katika wilaya hiyo kwani inauhitaji wa wawekezaji katika Nyanja mbalimbali.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Bukombe George Lutengano 

Rai hiyo ameitoa alipokuwa ofisini kwake hivi karibu ambapo amesisitiza kuwa wilaya ya Bukombe ina kila aina ya raslimali zenye kuwafanya kuweza kuja kuwekeza katika wilaya ya Bukombe.

Alisema kuwa Wilaya ya Bukombe imezungukwa na madini mengi sana hivyo ni wakati wa mashirika mbalimbali kuweza kujitokeza kwa wingi ili kuja kuwekeza katika uchimbaji wa madini, kilimo cha mazao ya chakula na  yale ya Biashara na pia katika ufugaji wa mifugo ya aina yote kwani malisho yapo na yenye uhakika.

Aidha Mkurugenzi Lutengano amewata wananchi wa Bukombe ambao wanaishia nje na Bukombe kutumia pia mahusiano yao kuweza kuwashawishi marafiki zao kuweza kuja na kuwekeza Bukombe na hata wao ni wakati wao sasa kuwekeza nyumbani kwao ili kubadilisha mazingira.

“Bukombe ya sasa sio ile ya miaka ya nyuma kwani sasa hivi kuna miundombinu ya uhakika na yenye kuvutioa kwa wawekezaji” Alisema Lutengano.

Kwa upande wake Michael Ally  mmoja wa wawekezaji wa mifugo Wilayani humo amewataka wawekezaji kuja Bukombe kwani  kuna Amani kubwa na nafasi za kutosha katika Nyanja ya uwekezaji.

Aidha aliongeza kuwa Bukombe kuna kila aina ya uwekezaji kikubwa ni ubunifu tu wa nini kifanyike na kufuata utaratibu wa uwekezaji kwa serikali yetu

MWISHO

Post a Comment

0 Comments