Na Shushu Joel, Bukombe
WANANCHI wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamempongeza Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko kwa utendaji kazi wake wa kuwaletea maendeleo ambayo miaka ya nyuma yalikuwa ni changamoto kubwa sana.
Wakizungumza na HABARI MPYA MEDIA Wananchi hao wamefunguka mengi huku wakidai kuwa kwa muda ambao Mhe Dkt Biteko amekuwa madarakani hakuna ambacho tunamdai kwani amefanikisha kulibadilisha jimbo la Bukombe kwa asilimia 100% .
Alexander Mtuzya ni Mkazi wa kata ya Bulangwa alisema kuwa Bukombe wamepita wabunge wengi ingawa walifanya kwa nafasi zao ila Dkt Biteko ametia fola kwa utendaji jambo ambalo limepekea wananchi wa Bukombe kutomdai kitu cha maendeleo.
Aliongeza kuwa Dkt Biteko amekuwa ni kiongozi mwenye kupenda haki ,upendo na muunganiko jambo ambalo limekuwa na mafanikio makubwa kwa jamii.
Naye Amina Hamis Mkazi wa kata ya Uyovu amempongeza Mbunge kwa jinsi ambavyo amekuwa kiungo cha wananchi wa Bukombe katika nyanja mbalimbali.
Hivyo kutokana na matendo mema ambayo yamekuwa yakifanywa na Dkt Biteko ni haki kusema wananchi wa Bukombo hakuna tunachomdai Mbunge wetu kwenye masuala ya maendeleo.
MWISHO
0 Comments