Na Shushu Joel, Bukombe
VIJANA wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wanashangazwa na utendaji kazi mkubwa wa maendeleo unaofanywa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Mashaka Biteko.
![]() |
Naiu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko akifafanua jambo (NA SHUSHU) |
Wakizungumza kwa wakati tofauti tofauti vijana hao walisema kuwa Wilaya ya Bukombe imekuwa na mabadiliko ya haraka sana kwenye nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
David Jelemiah ni mmoja wa vijana mkazi wa kata ya Katente mara baada ya kuzungumza na HABARI MPYA MEDIA alisema kuwa vijana wa Bukombe tunampongeza sana Mbunge wetu Dkt Biteko kwa jinsi ambavyo amekuwa akijituma na kuwaletea wananchi wa Bukombe maendeleo mbalimbali.
Aliongeza kuwa wabunge wengi wamepita ila Dkt Biteko amekuwa mfano na ni kiongozi mwenye maono ya mbali kwa maendeleo ya Taifa letu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya hiyo Nelvin Salabaga amewasifu vijana wa wilaya hiyo kwa kutambua thamani kubwa ya Mbunge hasa kwa maendeleo ambayo amezidi kuwafanyia wananchi wema wa jimbo la Bukombe, jambo ambalo lilikuwa ni kiu ya kila Mwananchi wa Bukomne kuona maendeleo yenye tija yakiganyika.
Aidha Mwenyekiti huyo amemuomba Dkt Biteko kuwafikishia salamu za pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa miaka 3 ambayo imezidi kuwa neema kwa wanabukombe na Watanzania kwa ujumla kwani hakuna sekta ambayo haijaguswa na Dkt Samia.
Hivyo ameeleza kuwa wao kama vijana wa Bukombe wataendelea kumsemea mema kwa wananchi kwani maendeleo ambayo anayafanya ni kielelezo tosha kuwa yeye ni kiongozi wa maendeleo na sio porojo.
MWISHO
0 Comments