WANAWAKE BUKOMBE WAMPA TUZO RAIS DKT SSH.

 Na Shushu Joel, Bukombe.

Mwenyekiti CCM Wilaya ya Bukombe akikabidhi Tuzo ya Rais Dkt Samia SuluhuHassan kwa Mkuu wa Willaya hiyo Said Nkumba (NA SHUSHU JOEL)

WANAWAKE wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamekabidhi tuzo ya heshima kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kama kutambua mchango mkubwa unaofanywa na kiongozi huyo.


Wakikabidhi tuzo hiyo maalum kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Said Nkumba Wanawake hao walisema kuwa Tuzo hiyo wameitoa kwa kutambua mchango mkubwa anaofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Wananchi wa Tanzania.


Mwalimu Jazaa Komba ni Mwenyekiti wa shughuli za Mwanamke Day kwa kipindi cha muda wa miaka mitano mfululizo ndani ya wilaya ya Bukombe alisema kuwa kipindi hiki sherehe hizo zimekuwa bora sana  kutokana na kinamama wengi kujitoa na kutambua thamani ya siku hiyo.


Aliongeza kuwa sherehe za mwaka huu zimekuwa na kielelezo kikubwa kwa upande wa Wanawake na hasa katika utendaji wa kazi za ujenzi wa Taifa letu jambo ambalo limefanywa na Rais wetu Dkt Samia kwa vitendo.


" Miaka ya nyuma Wanawake tulikuwa nyuma sana kwa kuogopa kufanya mambo kwa hofu kumbe Mwanamke anaweza kufanya kazi za maendeleo akiwa kiongozi kuliko hata mwanaume" Alisema Mwl Komba.


Akipokea Tuzo hiyo ya heshima Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg, Said Nkumba alisema kuwa Wanawake wa Bukombe wameipa heshima kubwa Wilaya hiyo kwa kitendo cha kutoa Tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutambua kile kinachofanywa na Jemedari huyo katika uongozi wake.


Aidha amewahakikishia tuzo itamfikia Rais Dkt Samia bila kipingamizi cha aina yeyote ile.


Pia Nkumba amewakumbusha Wanawake kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguI ujao wa Serikali za Mitaa kwani kiongozi wetu mkubwa katika Taifa hili ametoa dira ya kuwa Mwanamke anaweza kuibadilisha jamii pale anapoaminika na kuwa kiongozi.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments