"WANAWAKE TAIFA LINAWATEGEMEA" DC BUKOMBE

 Na Shushu Joel, Bukombe 


MKUU wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndugu Said Nkumba amewakumbusha Wanawake wa Wilaya hiyo na Tanzania kwa ujumla kuwa Taifa linawategemea kwa asilimia kubwa katika nyanja mbalimbali za  na ukuaji wa uchumi wa Taifa hili 



Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na umati wa wanawake waliojitokeza kwenye sherehe za siku ya mwanamke duniani ambapo kiwilaya ya Bukombe aya kwnye nviwanja vya sabasaba jijiDar Es akam,m


Nkumba alisema kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa wanawake wa Bukombe ni jeshi kubwa hivyo amekuwa akitililisha miradi mingi ya kutosha ili kumaliza changamoto zinazowakabili wanawake kama vile huduma za Afya, Maji, Miundombinu ya Barabara , Umeme hii yote ni kuonyesha jinsi gani Rais Dkt Samia anavyowathamini wanawake wa Bukombe.


Aidha aliongeza kuwa ni vyema tukatumia muda huu kuonyesha umoja ,upendo na mshikamano wetu wanawake katika muda huu ambako tunaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa. 


Pia DC Nkumba alisema kuwa maendeleo yote mnayoyaona ni uwakilishi mzuri unafanywa na Mbunge wenu ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Mashaka Biteko huko Bungeni .


Naye mratibu wa maadhimisho ya siku ya Mwanamke Dunia Bi, Mariana Genya amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuthamini kundi kubwa la Wanawake .


Aidha wanawake hao wamemuomba Mkuu huyo wa Wilaya kufikisha salamu zao kwa Mbunge Dkt Biteko na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia kuwa hatutomwangusa na ikiwezekana huku Bukombe asifanye kampeni kwani maendeleo aliyoyafanya ni kielelezo tosha .


MWISHO

Post a Comment

0 Comments