Na Shushu Joel, Chalinze.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Abdulsharifu Zahoro ameipongeza halmashauri ya Chalinze kwa jinsi ambavyo imekuwa imara katika usimamizi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.
![]() |
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo akifurahia jam |
Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani wa Chama hicho Mwenyekiti huyo alisema kuwa CCM imepitia miradi mingi katika halmashauri ya Chalinze na yote ikitekelezwa na mapato ya ndani jambo ambolo limekuwa na tija kubwa kwa wananchi .
"Tumepitia miradi ya Soko, Duka la dawa ambalo linamilikiwa na kituo hicho jambo ambalo lina tija kwa wakazi wa kata ya Bwilingu, Shule ya Msingi Ridhiwani Kikwete na Jengo la Mama na Mtoto lilipo kata ya Miono" Alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Sharifu.
Aidha amewakumbusha watumishi wa halmashauri hiyo kuzingatia weredi wa majukumu yao kisawasawa kwani fedha zinazotolewa na serikali ni kodi za wananchi hivyo wananchi wanahitaji kuona miradi yenye ubora na inayoendana na thamani ya fedha inayotolewa.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Halima Okash amemwakikishia Mwenyekiti wa CCM kuwa serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga kisawasawa juu ya usimamizi wa miradi hivyo kama msimamizi wa miradi wilaya ya Bagamoyo atahakikisha miradi yote inakwenda kama ilivyokusudiwa kwa wananchi.
Aidha Okash amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuzidi kuijali wilaya ya Bagamoyo kwani fedha ni nyingi zinazidi kuja kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
MWISHO
0 Comments