MKENGE AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUMUOMBEA DUA RAIS SAMIA.

 Na Shushu Joel, Bagamoyo 

MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoani Pwani Mhe. Mharami Mkenge amewataka viongozi wa Dini wilaya humo kuendeleza kutoa dua kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwa na Afya njema ili azidi kuwatumikia watanzania.

Mbunge wa Bagamoyo Mharamu Mkenge akialimiana na baadhi ya wajume mara baada ya iftyari ( NA SHUSHU JOEL)

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali na wananchi nyumbani kwake Bagamoyo ambapo alikutana na watu kwenye Iftari iliyoandaliwa na mbunge huyo .


Mkenge alisema kuwa Wilaya ya Bagamoyo ina historia kubwa katika Taifa hili na hasa kwa utoaji wa dua kwa viongozi wetu wa kitaifa hivyo naamini kuwa dua hii itakuwa ni kinga kwa viongozi wetu wa kitaifa na hivyo inakwenda kuwa nguzo kwa viongozi kwa wale wenye chuki na viongozi wetu.


" Namshukuru Mungu kwani nilihitaji watu 200 tu kwa iftari lakini wamefika watu zaidi ya Mia tabu (300) na ajabu kila kitu kimetosha kitu ambacho namwachia Mungu peke yake pia katika iftari yetu dua yetu imekubali kwani mvua kubwa imenyesha" Alisema Mhe Mkenge. 


Aidha Mbunge huyo ametumia nafasi hiyo kusema kuwa upendo alionao kwa wananchi wa Bagamoyo ataendelea kutoa iftari kwa watu mbalimbali ikiwemo wenye uhitaji.


Naye Mmoja wa Wananchi wa wilaya ya Bagamoyo Ibrahimu  Gama alisema kuwa Mhe. Mbunge Mkenge amefanya jambo kubwa sana kwetu wananchi wa wilaya ya Bagamoyo hivyo nasi tutaendelea kumuombea Dua jema kwa Mungu ili kila mwaka ndani ya mfungo mtukufu wa Ramadhani azidi kufanya jambo.


Aidha Gama amempongeza Mbunge kwa namna jinsi ambavyo amekuwa akifanya juhudi zake za utoaji wa iftari na ugawaji kwa watu wenye mahitaji maalum.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments