"DKT BITEKO NI NGUZO YA BUKOMBE "WANANCHI

 Na Shushu Joel, Bukombe 


WANANCHI wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wamempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko kwa jinsi ambavyo amekuwa nguzo ya maendeleo kwao.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko akifafanua jambo ( NA SHUSHU JOEL)


Salma Hamis ni mkazi wa kata ya Bulangwa alisema kuwa kwa kipindi kirefu sana jimbo hilo lilikuwa na changamoto za upatikanaji wa huduma muhimu za jamii lakini tangu Dkt Biteko ashike kijiti wananchi tumekuwa na maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali.


Aidha aliongeza kuwa sio tu sekta ya bali Dkt Biteko amefanikisha kutuunganisha wananchi wa Bukombe kwa wote kuwa chama chama kimoja cha maendeleo ambacho ni Chama Cha Mapinduzi (CCM)


Naye Joshua Mateng'e amemsifu Dkt Biteko kwa kuwa nguzo ya vijana katika kupiga kazi za maendeleo.


Pia aliongeza kuwa Vijana wa Bukombe tumejipanga ili kuhakikisha viongozi wetu wa kitaifa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan anapata ushindi mkubwa na mnono kuanzia ngazi za serikali za mitaa mpka yeye mwenyewe.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments