CCM YAZIDI KUPUKUTISHA UPINZANI BUKOMBE.

Na Shushu Joel, Bukombe 

CHAMA Cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kimezidi kuvuna wanachama kutoka vyama pinzani hii yote inatokana na ubora wa uongozi uliopo na utekelezaji wa miradi mbalimbali kuzidi kufanyika chini ya Mwenyekiti wake wa Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.


Akizungumza kwenye kikao kazi cha Wanawake wa kata ya Uyovu  katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya hiyo Ndugu Teddy Mageni alisema kuwa  Wanawake ni jeshi kubwa na lenye kutegemewa na CCM hivyo ni vyema kila Mwanamke kuongeza juhudi za kuongea na wanawake wenzetu ili kuhakikisha Rais wetu Dkt SSH a AVUNJA recodi ya upataji wa kula .


Aidha aliongeza kuwa CCM imezidi kujiongezea wanachama kutoka vyama pinzani hii yote ni kutokana na utendaji mkubwa unaofanywa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi katika maeneo yetu ya Bukombe.


Pia Katibu huyo amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko kwa maendeleo makubwa anayoyafanya kwa wananchi. 


" Bukombe ya sasa imekuwa na mabadiliko makubwa katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo Afya,Elimu, Maji, Umeme na Miundombinu yote hii ni juhudi za Dkt Biteko " Alisema Katibu wa UWT Mageni .


Kwa upande wake mmoja wa waliorudisha kadi ya Chadema na kujiunga CCM Bi, Mariam Humli amesema kuwa ameamua kurudi nyumbani kutokana na kile kinachofanywa na Mbunge Dkt Biteko kwani kukaa huku ni aibu kubwa.


Aliongeza kuwa kuna watu wengi watarudi Sema wanaona aibu lakini mioyo yao yote ipo Chama Cha Mapinduzi na watarudi tu mudi si mrefu.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments