Na Mwandishi wetu, KATAVI
Vijana wameaswa kuchangamkia fursa zitolewazo na serikali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi huku wakiaswa kutunza mazingira ili kuepuka athari ziletwazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Wito huo umetolewa na Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2024 Geofrey Mnzava,wakati akikagua shughuli za kikundi cha Vijana Gift kilichopo kata ya Kasekese Halmashauri ya Tanganyika Mkoani Katavi,wanao miliki mashine ya kukamua mafuta ya alizeti na duka la kuuza mafuta hayo.
Amewataka kuendelea kujisimamia na kuweka nidhamu katika kipato wanachokipata ili waendelee kujikwamua na kupiga hatua kutoka kwenye ujasiriamali wa kiwanda kidogo na kufika kwenye ujasiriamali mkubwa.
Mwenge wa uhuru umetembelea na kuzindua miradi 9 katika kata 6 ndani ya Halmashauri ya Tanganyika yenye thamani ya Bilioni 2.8.

0 Comments