Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya Bagamoyo Bw Aboubakary Mlawa amemuhakikishia Katibu Mkuu wa wazazi Taifa Bw Ally Hapi kuwa Chama cha mapinduzi kipo salama na kitaendelea kuwa salama.
![]() |
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Ndg Hapi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Bagamoyo Mlawa( Na Shushu Joel) |
Akitoa salamu za Chama na Jumuiya wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu hyo Mlawa alisema Kamati ya siasa inaendelea kusimamia sSetikali na kuleta amani na ushirikiano wa wanachma kama kawaida na hasa kipindi hiki ambacho Mwenyekiti wa Chama wilaya kutokuwepo kutokana na kuvuliwa Uongozi na Kamati kuu ya CCM Taifa.
"Ndugu Katibu Mkuu pmoja na jahazi la uongozi kukumbwa na dhoruba nna Nahodha kuishia njiani lakini manahodha wengine tupo na chombo kitaendelea na safari "Alisema Mlawa.
Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wazazi Taifa Ndugu Ally Hapi aliwataka ushirikiano na miakikakati iwepo kwa ajili ya chaguzi zilizo mbele za aerials ta Mitaa.
Akisema si muda muafaka wa kujadili kimetokea nini na sababu gani,bali wanaccm ni wakati wao kuonyesha ushirikiano na kupanga mikakati ya kuhakikisha Chama kinashinda kwa kishibdo.
0 Comments