"VIONGOZI ACHENI MBWEMBWE, PIGENI KAZI" HAPI


Na Shushu Joel, Kibaha. 


KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi (CCM) Taifa Ndugu Ally Hapi amewataka viongozi wa jumuiya hiyo na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha wanashuka chini na kufanya mikutano na wananchi.


Hayo ameyasema alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Chama na Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili ofisi za ccm.

Katibu Mkuu wa wazazi Taifa Ndugu Ally Hapi akizungumza na viongozi mbalimbali waliojitokeza kwenye kikao Mkoani Pwani ( Na Shushu Joel) 

Alisema kuwa viongozi wengi tumekuwa na Mbwembwe tu na kushindwa kuwaeleza wananchi kile ambacho kimefanywa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan. 


" Jambo jema kila kiongozi akachakalika  kufanya mikutano ya ndani na ile ya hadhara huku tukielezea maendeleo yanayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan " Alisema Katibu Mkuu wa wazazi Ndugu Hapi.


Aidha Katibu Mkuu wa Wazazi Taifa Ndugu Hapi amewakumbusha viongozi kuwajibika kwa dhati kwa wananchi ili waendelee kukipenda Chama Chao.


Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani Ndugu Jackson Kituka amemwakikishia katibu Mkuu kuwa Mkoa wa Pwani unaenda kupata ushindi wa kishindo katika chaguzi zote hii ni kutokana na umoja na upendo walionao.


Aidha amesema kuwa Mkoa wa Pwani unaenda kuweka rekodi kwa kumpigia kura za kishindo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan hapo mwakani.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments