Na Shushu Joel, Bagamoyo
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndg Ally Hapi amewataka viongozi na wana chama wa Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha wanawachagua viongozi wenye sifa na wanao kubalika kwa jamii.
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kata ya Miono Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Taifa Ndg Hapi yupo katika ziara ya kikazi Mkoa wa Pwani ambapo anakutana na viongozi na wananchi mbalimbali kwa lengo la kuwakumbudha umuhimu wa kukichagua Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuwatumikia na kuwaletea maendeleo.
" Viongozi wenye kukubalika kwa jamii ndio wanaoutajika hivyo ni vyema kuwachagua ili waweze kupeperusha bendera ya chama chetu " Alisema Hapi
Aidha amewatamba wana CCM kutembea kifua mbele kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM anafanya mambo makubwa ya maendeleo katika Taifa hili.
Kwa upande wake Katibu wa Siasa na itikadi Mkoa wa Pwani David Mramba amempongeza Katibu Mkuu Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Taifa Ndg Hapi kwa kufanya ziara katika Mkoa kitu ambacho kimeongeza tija kubwa Mkoa wa Pwani.
Aidha Mramba amewakumbusha wananchi wa Mkoa wa Pwani kukipigia kura Chama cha Mapinduzi katika chaguzi zote zinazokuja .
"Kila mmoja wetu ni muhimu kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa " Alisema Katibu Mwenezi Mkoa wa Pwani Ndugu Mramba.
MWISHO
0 Comments