HAJAT MARIAM ULEGA AONGEZA NGUVU USAJILI WA WANACHAMA KIELEKTRONIKI CCM- UWT SHINYANGA


Na Mwandishi wetu 



Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake  wa Chama cha Mapinduzi 

(UWT) Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega amechangia Simu tatu ili kuongeza nguvu ya Kusajili Kielektroniki Wanachama wa CCM kupitia UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini.


Ndugu  Mariam Abdallah Ulega ametoa msaada huo leo Jumatatu Oktoba 7,2024 kwenye Kikao cha Viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wakati akiwa ziara yake ya Kuhamasisha zoezi la kusajili wanachama wa CCM Kielektroniki ikiwa ni sehemu ya kuunga Mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuimarisha CCM.


“Sisi wote wanaCCM ni ndugu, tunaimarisha chama chetu na tunaendelea kukijenga zaidi. Kwa kasi yenu ya Usajili hapa ninavyoiona na nguvu kubwa mnayotumia kuhakikisha tunapata wanachama wengi zaidi katika chama chetu cha Mapinduzi, Na mimi nimewiwa kuongeza nguvu kwa UWT, nakabidhi simu hizi tatu ili tuendelee na zoezi la usajili kwa wale ambao bado hawajajisajili Kielektroniki”,amesema Mariam.


 “Lakini nataka niwaambie viongozi wenzangu hima hima twende tukahimizane tujiandikishe na tuhakikishe tunaboresha taarifa zetu katika Daftari la Wapiga kura,  wale ambao hawajiandikisha kwenye daftari wakati ni sasa daftari lipo, tuzidi kuhakikisha tunakuwa na viongozi bora ambao watakuja kuchukua fomu katika uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo tunakuwa na wanachama ambao wapo hai na wapo kindakindaki kukipigania chama chetu”,ameongeza Mariam.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe ,Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Chacha na  Katibu wa UWT Shinyanga Mjini Getrude Mboyi wamemshukuru Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Mariam Abdallah Ulega kwa kuwaongezea nguvu kwa kuwapatia vitendea kazi huku wakieleza kuwa zoezi la kusajili Kielektroniki wanachama CCM linaendelea vizuri.


****

Post a Comment

0 Comments