SERIKALI KUONGEZA NDEGE NYUKI  KUDHIBITI WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU-WAZIRI PINDI CHANA


Na IRENE TEMU , Katavi 


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema Wizara imeendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kudhibiti changamoto za Wanyamapori wakali na waharibifu huku akisisitiza mkakati wa kuongeza ndege nyuki ili kudhibiti tembo.


Waziri  Chana  ametoa kauli hiyo leo  Oktoba 3,2024 wakati  akizungumza na Watumishi wa Hifadhi ya Taifa Katavi katika Makao Makuu ya Hifadhi hiyo yaliyopo kata ya Sitalike Halmashauri ya Nsimbo,Mkoani Katavi.


Amesema Mh.Rais tayari ameelekeza kudhibiti wanyama wakali ikiwemo tembo hivyo amehamasisha vijana katika vijiji vilivyoko pembezoni mwa maeneo ya hifadhi kujitokeza kujiandikisha kupata mafunzo hayo ya kudhibiti Wanyamapori wakali na waharibifu.


Aidha Waziri Chana amesema Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kujenga vituo vya askari kuhakikisha kuna uhifadhi endelevu na kudhibiti Wanyamapori wakali.

Post a Comment

0 Comments