Na Shushu Joel, Geita
UMOJA wa Vijana Mkoa wa Geita wamempongeza Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ndugu Manjale Magambo kwa jinsi ambavyo amekuwa kiongozi mwenye maono ya mbali katika kukuza jumuiya hiyo.
![]() |
Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Geita Ndugu Manjale akifafanua jambo |
Umoja wa Vijana Mkoa wa Geita umepiga hatua kubwa katika shughuli mbalimbali za jumuiya ikiwemo mafunzo ya ukakamavu kwa vijana kwenye Wilaya zote za Mkoa huku Hamasa kubwa ikitolewa na Mwenyekiti huyo .
Nelvin Salabaga ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kutokea Wilaya ya Bukombe anasema kuwa viongozi wenye maono kama ya Manjale ni wachache kwani amekuwa ni kiongozi kimbilio kwa vijana wa rika lolote ndani ya Mkoa wa Geita.
Aidha amewataka vijana ndani ya Mkoa kuendelea kumuombea kwa Mungu ili azidi kumpa Afya njema kwani Jumuiya yetu ameibadilisha sana huku akidai anataka lazima Vijana wa Geita wawe wa Mfano hapa Nchini.
Naye Devid Jeremiah amewataka vijana kutembea kifua mbele kwani yajayo kwa upande wa vijana kupitia Mwenyekiti wetu wa Mkoa Ndugu Manjale yanafurahisha sana katika Jumuiya.
Aidha Devid amemuomba Mwenyekiti kuwasaidia vijana kuwawezesha ili waweze kukuza uchumi wao kwa kufungua kitegauchumi ambacho kitawawezesha vijana kukua kiuchumi zaidi.
MWISHO
0 Comments