Na Shushu Joel, Geita
MTOTO wa Hayati John Pombe Magufuli Bi, Jesca Magufuli amewashushia neema uongozi wa Umoja wa Vijana Mkoa (UVCCM) kwa kugawa pikipiki kila Wilaya za Mkoa huo.
![]() |
Jesca Magufuli akimkabishi katibu wa Uvccm Mkoa wa Geita nyaraka za pikipiki (Na Shushu Joel) |
Akizungumza wakati wa kukabidhi Pikipiki hizo Bi, Jesca alisema kuwa yote hayo aliyoyafanya ni kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha Bi, Jesca alisema ni vyema pikipiki hizi zikatumike kwa lengo ambalo limekusudiwa ili ziweze kuleta tija kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hasa vijana wenzetu.
"Chama chetu cha Mapinduzi kitazidi kuwa imara kwa kuendeleza umoja wetu tulionao" Alisema Jesca Magufuli
![]() |
Pia amewakumbusha viongozi wa Vijana wa Mkoa na Wilaya kuendelea kumsemea Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa nguzo ya maendeleo katika Taifa letu .
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kutokea Wilaya ya Bukombe Ndugu Nelvin Salabaga amempongeza Jesca Magufuli kwa msaada wake alioutoa kwa jumuiya hivyo sisi kama vijana tutaendelea kumuunga mkono kwa juhudi Zale anazozifanya kwetu.
MWISHO
0 Comments