Na Shushu Joel, Chato
MBUNGE wa Mkoa wa Geita Mhe Josephine Chagula amegawa mashuka katika kituo cha Afya cha Kachwamba kilichopo Wilaya ya Chato Mkoani Geita
Akizungumza wakati wa kukabidhi mashuka hayo Mhe Chagula alisema kuwa nimeamua kutekeleza ahadi yangu ambayo nilitoa miezi michache iliyopita nilipopita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi mwenye uchu mkubwa wa mafanikio kwa Taifa lake Hivyo amekuwa akitekeleza kwa vitendo miradi mbalimbali.
Aidha amewataka watumushi wote wa kituo hicho kuhakikisha wanazitumia shuka hizo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa jamii ili yaweze kufanyika.
Pia katika ziara hiyo Mhe Mbunge Chagula ametoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa kwenue hodi mbalimbali ikiwemo ya wazazi na ile ya watoto wilayani Chato.
Naye Mganga Mkuu wa kituo hicho Dr Paschal Kulwa amempongeza Mhe.Chagula kwa msaada huo wa mashuka kwani awali walikuwa na upungufu lakini kwa msaada huo wa Mbunge wa mashuka 50 unaondoa kabisa changamoto hiyo
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ya kachwamba Bi, Stela Masabile amemshukuru Mbunge wa viti maalum kwa msaada huo wa mashuka ambao utatumika kwa wagonjwa mbalimbali watakaokuja kupata huduma katika kituo cha Afya hicho.
MWISHO


0 Comments