Na Shushu Joel, Katoro
MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Geita Mhe Josephine Chagulla amegawa gesi kwa Mama Lishe wa katoro kwa lengo la kuondoka na upishi wa kutumia Mkaa na kuni.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mhe Chagulla alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa ikipambana na suala la kuondoa matumizi ya Mkaa na badala yake watu waweze kutumia Nishati safi na salama.
"Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan ana malengo makubwa na mathubuti juu ya matumizi ya Nishari bora na ifikapo 2030 asilimia kubwa ya watanzania wawe wanatumia Nishati safi na salama" Alisema Mhe Josephine Chagula
Aidha amewataka Mama Lishe hao kuwa mabalozi kwa wengine ili nao waweze kuhamia katika matumizi sahihi kwa Nishati Safi na Salama.
Naye Mmoja wa wanufaika wa Majiko hayo ya Gesi ambaye ni Mama Lishe ambaye amejitambulisha kwa jina la Mama Juma alisema kuwa kwa Mama lishe kuwezeshwa kupata majiko ambayo yanakwenda kuondoa matumizi ya Mkaa na kuni.
Aidha amempongeza Mbunge Mhe. Josephine Chagulla kwa kuwaona Mama Lishe wawe wanufaika wa matumizi ya Nishari safi na salama.
MWISHO
0 Comments