NI AIBU KUWAPA KURA UPINZANI M/KITI WAZAZI BUKOMBE


Na Shushu Joel, Bukombe 


WENYEVITI  wa jumuiya tatu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM),Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) na jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita umeanza ziara ya kishindo Wilaya hiyo kwa kusudi la kukutana na makundi yote matatu na kuwakumbusha kila kundi kuweza kuwajibika kwa wananchi.

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Bukombe Ndugu Hassan Mohamed alisema kuwa kutokana na jinsi ambavyo Mbuge wa Jimbo ambaye ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko amekuwa akishusha miradi ya maendeleo kwa jamii sidhani kama kuna mpinzani atapata kura hata moja.


Aliongeza kuwa Wananchi wa Kata ya Namonge  wanakumbuka jinsi walivyokuwa na changamoto kipindi cha nyuma ambapo kata hiyo ilitawaliwa na Upinzani Hivyo ni vyema kuendelea  kuipa nafasi ccm iendelee kushika dola kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa. 


Aidha Mwenyekiti huyo wa Wazazi amewakumbusha wanaccm kuendelea kutembea kifua mbele kwani serikali ya chama cha mapinduzi chini ya Mwenyekiti wa Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kimefanya mambo makubwa.


Kwa upande wake Mzee maarufu wa kata hiyo Samweli amempongeza Mwenyekiti wa Wazazi huku akimhakikishia kuendelea kuwa na amani hakuna kijiji wala kitongoji kitakachopotea.

 

MWISHO

Post a Comment

0 Comments