Na Shushu Joel, Bukombe
AGIZO alilolitoa Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko limetekelezwa kwa asilimia zaidi ya 90 na uongozi wa kijiji cha Ilyamchele kata ya Namonge Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.
Agizo ambalo alilitoa Dkt Biteko katika kijiji hicho alipokuwa kwenye ziara jimboni kwake ilikuwa ni kukarabatiwa upya zahanati ya kijiji hicho na hivyo jambo hilo limefanywa kwa haraka na kwa wakati kwa lengo la utoaji wa huduma za Afya uweze kufanyika.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo Mhe Diwani Ndugu Mlalu Bundala alisema kuwa kabla ya ukarabati wa zahanati hiyo ilikuwa ni ya kawaida sana lakini agizo na msaada mkubwa wa fedha na vifaa uliofanywa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu.
Aidha Diwani hiyo amempongeza Dkt Biteko kwa jinsi ambavyo amekuwa kimbilio kwa wananchi wa kata ya Namonge na hasa kwenye maendeleo jambo ambalo limezidi kuwapa matumaini makubwa wananchi ikilinganishwa na kule walikotoka.
" Mpaka sasa tumepokea zaidi ya milioni 4 huku ahadi ikiwa ni milioni 10 kwa ajili ya kumalizia zahanati hiyo ili iwe ya kisasa " Alisema Diwani Mhe. Mlalu
MWISHO
0 Comments