Na Shushu Joel, Bukombe
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (Uvccm) Wilaya ya Bukombe Ndugu Nelvin Salabaga amesema kuwa Uchaguzi wa Serikali za mtaa, Vijiji na Vitongoji ni dira ya uelekeo wa uchaguzi Mkuu kwa Chama Cha Mapinduzi (ccm)
Hayo ameyasema alipokuwa akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na wagombea wa nafasi za uenyekiti wa Mtaa, Vijiji na Vitongoji katika kikao maalum katika kata ya Runzewe Magharibi Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.
Aliongeza kuwa Chama Cha Mapinduzi kikishinda nafasi nyingi kwenye nafasi za uchaguzi wa serikali za mtaa ndio dira kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais ,Wabunge na Madiwani ,Hivyo ni vyema kila mtu kuendeleza hamasa kwa jamii ili kuweza kuipigia kura ccm.
Aidha alisema kuwa kwa kipindi hiki cha uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni maendeleo mengi yamefanyika katika Taifa hili hivyo sioni mpinzani atakayechukua fomu ya kuomba nafasi yeyote labda kama anataka kujitia aibu ya kukosa kura.
"Endeleeni kuyasema maendeleo yanayofanywa na Mbunge wetu ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko" Alisema Mwenyekiti Nelvin
Pia amewakumbusha wananchi wa Jimbo la Bukombe kuweza kuwa na kumbukumbu ya kule tulikotoka na tulipo sasa chini ya Dkt Biteko.
Naye Daud Seme ambaye ni barozi amempongeza Mwenyekiti wa umoja wa vijana kwa maneno yaliyoenda shule huku akimwakikishia Mwenyekiti huyo kuwa katika kata ya Runzewe Magharibi hakuna Mtaa,Kijiji wala Kitongoji kitakachopotea kwani kila mtu anaona kile kinachofanywa na Viongozi wetu akiwemo Mbunge wetu Dkt Biteko.
MWISHO
0 Comments