Na Shushu Joel, Bukombe
VYAMA vya Upinzani Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita vimeamua kujifungia ndani mara baada ya kusikia kufanyika kwa ziara ya hatari ya Wenyeviti watatu wa Jumuiya tofauti tofauti katika Kata mbalimbali za Jimbo hilo.
Akizungumza na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kunazia ngazi ya shina mpaka kata,mabalozi, wanachama wa kawaida na wale waliopewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye nafasi ya uenyekiti wa kijiji,mtaa na kitongoji.
Kiongozi wa msafara huo ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Ndugu Hassan Mohamed alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwakumbusha kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwani kimefanya maendeleo makubwa na yasiyo na kifani katika Taifa .
Aidha Mwenyekiti huyo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kushusha fedha za kutosha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa Uvccm Bukombe amewataka vijana kuendelea kumsemea Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko kwa yale ambayo anatufanyia wanabukombe.
Naye Mwenyekiti wa Wanawake Bi, Julieth Simon amewakumbusha Wanawake kutembea kifua mbele kwani Mwanamke mwenzetu ambaye ni Rais wetu Dkt Samia ametuheshimisha sana wanawake Hivyo tumpe heshima kwa kuwapa kura wenyeviti wa ccm
MWISHO
0 Comments